Thursday, April 11, 2013

Growing up in the 90s (Swahili Version)




Kwa ndugu zangu wazungumzao Kiswahili.

Ninapofikiri kuhusu utoto wangu najifikiria kama kile kizazi cha Mwinyi/Mkapa kile kizazi tulikua na kuimba nyimbo kama vile “kwaheri mwalimu, kwaheri mwalimu” pindi tuionapo ndege angani. Kilikuwa kizazi kionacho furaha kwenye kila kitu. Hatukuwa na Facebook, lakini mara zote tulikuwa na njia za kutuunganisha na marafiki zetu.




Tulikuwa hodari katika kucheza mchezo wa kurungusha ringi na kuendesha gari za waya. Hatukuhitaji kwenda masoko ya kisasa kununua mipira tulichohitaji ni vikasha vitupu vya kuwekea maziwa na kamba za mipira. Kirahisi tulikuwa wabunifu.

Miaka ya 90 ilikuwa na  madaraja kidogo ya ufaulu wa juu, stashahada kidogo ya madaraja ya kwanza lakini kulikuwa na watu wengi wapatao kazi. Ukosefu wa kazi haukusikika. Shule haikuwa kuhusu kutoka wakwanza. Wote tulikimbiza mbio zetu: Kiu ya wote ilikuwa ni kupata elimu. Nilijifunza kusoma na kuandika Kiswahili chekechea, huko kijenge. Ilikuwa ni sababu ya bidii za mwalimu wangu wa darasa la awali mwalimu mmoja Harriet, alimpa kazi.

Tukirudi nyumbani tulikuwa na stesheni moja ya televisheni lakini tulipata elimu Zaidi kutoka huko. Kuna kumbukumbu tamu za shangazi yangu aliyepita akitupa vijikazi vya kumpa muhutasari wakile Rainfred Masako alikisema kwenye wasaa wa habari. Kibanzi hakikuwa mbali na nyumba. Yoyote mkubwa kwako aweza kukuweka bakora kutoka huko. Tuliheshimu kila mtu. Tulifahamu majirani zetu wote kwa majina. Kulikuwa na huo muunganiko ndani ya eneo. Siwezi sahau mikutano ya baraza la kijiji mara moja kila katikati ya mwezi, mama hunichukua tuongozane. Hatukuwa na “I – pads” lakini tuliweka kitabuni dondoo zinazohusu jamii.

Hatukuwa na migahawa mingi ya chakula lakini mara zote tulipata chakula bora. Ingawa tulikuwa na madaktari wasio tosheleza, watu wachache walikufa na magonjwa ya kisasa. Kisukari na Saratani zilikuwa hadimu miaka ya 90. Kama mototo, menyu ya chakula kwenye familia yetu ilikuwa na machaguzi mawili kula au kutokula. Sivyo kama ilivyo leo watoto waki washuruti wazazi wao kila pande.

Tukiongelea kuhusu uwajibikaji wa polisi kwenye dharura. Nakumbuka nyuma nikiwa mwanafunzi shule ya msingi darasa la kwanza niliwachezea mzaha polisi. Nilikwenda kwenye kibanda cha simu (kitumiacho sarafu) Posta kuu na kupiga simu niki igiza kulikuwa na wezi pale ofisi za posta. Ndani ya dakika chache polisi walifika.

Miaka ya tisini inazidi siku za sasa kwa kila namna. Tukizungumzia thamani iliyokuja na shilingi. Ndugu yangu mmoja wa mbali alnitembelea siku moja na kunizawadia shs1,000 na kwa wiki nzima nilipata shida “kumaliza” hiyo pesa. Nilikuwa na furaha utotoni hata michezo ya video, vikapu vya magurudumu katika masoko ya kisasa yaweza fananishwa na kipindi hiko kikubwa.

Kama ningekuwa na ndoto, ambapo ningeweza nyanyua fimbo ya maajabu na kufanya ziwe kweli, ninge tamani kuishi tena miaka ya 90.


for English version click HeRe.

1 comment: