Kwa ndugu zangu wazungumzao Kiswahili.
Ninapofikiri kuhusu utoto wangu najifikiria kama kile kizazi
cha Mwinyi/Mkapa kile kizazi tulikua na kuimba nyimbo kama vile “kwaheri
mwalimu, kwaheri mwalimu” pindi tuionapo ndege angani. Kilikuwa kizazi kionacho
furaha kwenye kila kitu. Hatukuwa na Facebook, lakini mara zote tulikuwa na
njia za kutuunganisha na marafiki zetu.
Tulikuwa hodari katika kucheza mchezo wa kurungusha ringi na
kuendesha gari za waya. Hatukuhitaji kwenda masoko ya kisasa kununua mipira
tulichohitaji ni vikasha vitupu vya kuwekea maziwa na kamba za mipira. Kirahisi
tulikuwa wabunifu.
Miaka ya 90 ilikuwa na
madaraja kidogo ya ufaulu wa juu, stashahada kidogo ya madaraja ya
kwanza lakini kulikuwa na watu wengi wapatao kazi. Ukosefu wa kazi haukusikika.
Shule haikuwa kuhusu kutoka wakwanza. Wote tulikimbiza mbio zetu: Kiu ya wote
ilikuwa ni kupata elimu. Nilijifunza kusoma na kuandika Kiswahili chekechea,
huko kijenge. Ilikuwa ni sababu ya bidii za mwalimu wangu wa darasa la awali
mwalimu mmoja Harriet, alimpa kazi.
Tukirudi nyumbani tulikuwa na stesheni moja ya televisheni
lakini tulipata elimu Zaidi kutoka huko. Kuna kumbukumbu tamu za shangazi yangu
aliyepita akitupa vijikazi vya kumpa muhutasari wakile Rainfred Masako
alikisema kwenye wasaa wa habari. Kibanzi hakikuwa mbali na nyumba. Yoyote
mkubwa kwako aweza kukuweka bakora kutoka huko. Tuliheshimu kila mtu.
Tulifahamu majirani zetu wote kwa majina. Kulikuwa na huo muunganiko ndani ya
eneo. Siwezi sahau mikutano ya baraza la kijiji mara moja kila katikati ya
mwezi, mama hunichukua tuongozane. Hatukuwa na “I – pads” lakini tuliweka
kitabuni dondoo zinazohusu jamii.
Hatukuwa na migahawa mingi ya chakula lakini mara zote
tulipata chakula bora. Ingawa tulikuwa na madaktari wasio tosheleza, watu
wachache walikufa na magonjwa ya kisasa. Kisukari na Saratani zilikuwa hadimu
miaka ya 90. Kama mototo, menyu ya chakula kwenye familia yetu ilikuwa na
machaguzi mawili kula au kutokula. Sivyo kama ilivyo leo watoto waki washuruti
wazazi wao kila pande.
Tukiongelea kuhusu uwajibikaji wa polisi kwenye dharura.
Nakumbuka nyuma nikiwa mwanafunzi shule ya msingi darasa la kwanza niliwachezea
mzaha polisi. Nilikwenda kwenye kibanda cha simu (kitumiacho sarafu) Posta kuu
na kupiga simu niki igiza kulikuwa na wezi pale ofisi za posta. Ndani ya dakika
chache polisi walifika.
Miaka ya tisini inazidi siku za sasa kwa kila namna.
Tukizungumzia thamani iliyokuja na shilingi. Ndugu yangu mmoja wa mbali
alnitembelea siku moja na kunizawadia shs1,000 na kwa wiki nzima nilipata shida
“kumaliza” hiyo pesa. Nilikuwa na furaha utotoni hata michezo ya video, vikapu
vya magurudumu katika masoko ya kisasa yaweza fananishwa na kipindi hiko
kikubwa.
Kama ningekuwa na ndoto, ambapo ningeweza nyanyua fimbo ya
maajabu na kufanya ziwe kweli, ninge tamani kuishi tena miaka ya 90.
for English version click HeRe.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete