Tuesday, May 15, 2012

Airtel yazindua Ofa ya SUPA 5....

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel ‘AIRTEL SUPA 5’ itakayotoa ofa tano kuwafaidisha wateja kuongea kwa NUSU Shilingi kwa sekunde siku nzima kwa marafiki Airtel-Airtel, pia wateja wote wataongea kwa ROBO Shilingi kwa sekunde usiku kucha Airtel-Airtel, kujipatia SMS 200 Bure Siku Nzima endapo mteja atatuma SMS10 tu kwa 30Tshs, facebook burepamoja na kuburudika intaneti ya bure usiku mzima kwa wateja wote.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Rahma Mwapachu akifafanua jambo jinsi ya kupata facebook bure kupitia ofa za AIRTEl SUPA 5 mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani). Hafla hiyo ya uzinduzi  huo umefanyika leo katika ofisi za Airtel Makao makuu, Ili mteja uweze kuingia na kutumia huduma hii unatakiwa kujiunga kwa kupiga *149*99#. Kisha utapata ujumbe utakaokuhitaji kuchagua muda maalum wa kutumia OFA hii yaani WIKI MOJA au SIKU MOJA, alafu utaweza kujaza namba zako maalum 3 za ndugu, jamaa, au rafiki utakazotaka kuwa unazipigia simu kwa NUSU shilingi siku nzima ndani ya muda wako wa ofa, Mbali na hilo huduma hii ya SUPA 5 inatoa nafasi kwa mteja yeyote wa malipo ya kabla wa Airtel ambaye amejiunga lakini pia muda wake ukiisha anaweza kujiunga tena kwa mara nyingine, lengo ni kumpa mteja wa Airtel nafasi ya kujiachia kwa unafuu na uhakika zaidi muda wowote na sehemu yoyote nchini Tanzania. Huduma ya Airtel SUPA 5 ni ya kudumu, lengo lake ni kutimiza mahitaji ya wateja wetu nchini bila kujali aina ya simu anayotumia huku tukitoa mawasiliano bora kupitia mtandao wetu ulionea kila mahali nchini Tanzania.
Jiunge na OFA hii ya Airtel SUPA 5 kwa kupiga *149*99#.

0 comments:

Post a Comment