Sunday, May 27, 2012

Stars yatoka sare na Malawi ndani ya Uwanja wa Taifa.....

Timu ya Taifa 'Taifa Stars' leo imeshindwa kutamba mbele ya Malawi katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya michezo ya kusaka tiketi ya kombe la dunia mwaka 2014 ambapo Taifa Stars itwakwaana na Ivory Coast na Malawi kuwavaa Waganda. Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na mchezo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana huku Taifa Stars wakifanya makosa ambayo yange igharimu timu hiyo hii leo kama Malawi wangekuwa Makini. Taifa Stars walicheza kiuwelewano katika kipindi cha kwanza na huku wakitengeneza nafasi chache za kujipatia magoli wakati wa Malawi walionekana kuwa hatari kwa mipira mirefu. Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa stars ambapo kuungo chake kilipotea na kadri ya dakika zilivyosogea wachezaji walionekana kuchoka. Nafasi pekee ambayo Stars wameijutia kuipoteza ilikuwa katika dakika ya 58 ambapo Shomari Kapombe na Mbwana Samata waligusiana vyema na mpira wa mwisho kumkuta Samata ambaye aliingia na mpira kwenye eneo la hatari akitokea upande wa kulia na alipo piga pasi ya chini chini kuelekea kwa Haruna Moshi 'BOBAN' ambapo beki wa Malawi ulimgonga na kwenda kugonga mwamba wa pembe ya pili na mpira kuamba katikati ya Boban na Ngassa kabla ya beki wa Malawi kuutoa nnje na kuwa kona. Na nafasi pekee ambayo wa Malawi wanaweza jutia ni ile ya kipindi cha kwanza ambapo Juma Kaseja alielekea upande sio baada ya Yondan kuhamisha muelekeo mpira katika purupushani ya kuokoa na mpira kumkuta mshambuliaji wa Malawi aliyepiga kichwa na mpira wake kuokolewa na Aggrey Morise.

0 comments:

Post a Comment