Friday, May 18, 2012

Mafisango afariki kwa Ajali ya Gari......

Enzi za Uhai wake akishangilia moja ya mabao aliyofunga
Gari aliyopata nayo ajali kama inavyoonekana
Mafisango alifariki dunia papohapo kwenye ajali wakati wakitoka Club kuelekea nyumbani,walipofika kwenye taa za barabarani Tazara Dar es salaam, Mafisango ambae ndio alikua anaendesha alijaribu kuziwahi taa lakini ghafla akakutana na mwendesha guta ambapo katika kumkwepa gari ilimshinda na kuingia mtaroni leo Alfajiri. Alikua na wenzake kwenye gari ambapo wengine wanne wamepona japokuwa walipata majeraha madogo madogo akiwemo mdogo wake ambae amesajiliwa na timu ya Simba. Mwili wa marehemu utaagwa kesho kwenye Viwanja vya TCC, kabla ya kusafirishwa Nyumbani kwao. Mafisango atakumbukwa kwa mengi aliyofanya katika Klabu yake ya Simba S.C, pamoja na Timu ya Taifa ya Rwanda. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi, Ameni!!!

0 comments:

Post a Comment