Saturday, May 12, 2012

Obama aunga mkono ndoa za jinsia moja

Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja .Rais Obama ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na idhaa ya kiingereza ya BBC.Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.
Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.

0 comments:

Post a Comment