Monday, March 19, 2012

ANC Yamtimua MalemaKiongozi wa mrengo wa vijana katika chama tawala cha ANC nchini Africa Kusini, Julius Malema, sasa ametimuliwa rasmi kutoka chama cha ANC baada ya rufaa ya kupinga uamuzi wa kutimuliwa kwake hapo awali, kutupiliwa mbali.
Kamati ya nidhamu ya chama cha ANC ilitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na Malema dhidi ya kutimuliwa kwake chamani kwa kipindi cha miaka mitano kwa makosa ya kuleta mgawanyiko katika ANC.
Kamati hiyo ikiongozwa na kiongozi mkongwe na mfanyibishara Cyril Ramaphosa, iliangalia tena rufaa aliyokata Bw Malema na bado ikampata na makosa ya kukigawanya chama cha ANC pamoja na kukitia aibu.
Hata hivyo, Malema katika siku za awali ameelezea wazi kwamba atakata rufaa iwapo kamati hiyo itamsimamisha kujihusisha na shughuli za chama tawala cha ANC.
Bw Malema bado anaweza kukata rufaa katika kipindi cha miaka 14.
Julius Malema amekuwa akisisitiza kuwa anaonewa kwa sababu anataka chama hicho kutaifisha migodi ya nchi hiyo.
Pia anasema baadhi ya watu katika chama cha ANC hawamtaki kwa sababu anataka chama hicho kupata kiongozi mpya katika mkutano wake baadaye mwaka huu ili kuchukua nafasi ya Rais Jacob Zuma kuondoka

0 comments:

Post a Comment