Friday, June 1, 2012

Lampard nje........Henderson ndani kuchukua nafasi yake

Kiungo wa Chelsea na England Frank Lampard amefeli kuweza kupona majeraha yake ya paja na ameondolewa kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Euro 2012 nchini Poland na Ukraine.Lampard, 33 alipata majeraha hayo kwenye mazoezi jana na alipewa taarifa mbaya na jopo la madaktari kufuatia vipimo alivyofanyiwa mapema leo. 
Kiungo wa Liverpool, Jordan Henderson atambadili Lampard kwenye kikosi cha Roy Hodgson.

0 comments:

Post a Comment