Kocha mpya wa timu ya taifa ya
Tanzania bara, Kim Poulsen amekosa kuwachagua katika kikosi chake
baadhi ya wachezaji wa muda mrefu wa timu ya taifa. Poulsen kutoka Denmark, amewachagua wachezaji wapya kuwa miongoni mwa wachezaji 22 wa timu ya Taifa Stars. Juhudi hizo ni miongoni mwa maandalizi ya kocha huyo kwa mashindano ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, Ameamua kuwatema baadhi ya wachezaji wenye uzoefu wa muda mrefu na kuwachagua vijana wadogo zaidi. "Nimeamua kuwachagua vijana hawa wadogo kwa kuwa ninaamini wataweza kuifanya kazi hiyo ya timu ya taifa", alielezea. Poulsen aliwahi kuifunza timu ya Tanzania ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 na vile vile miaka 20, kabla ya kurithi
kazi ya raia mwenzake wa Sweden, na ambaye majina yanafanana, Jan
Poulsen. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 ameamua
kutowaalika wachezaji wa zamani kama nahodha Shadrack Nsajigwa, Nadir
Haroub, Henry Joseph, Nizal Khalfan na Abdi Kassim. Kinyume na hayo, ameamua kumchukua tena
mshambulizi mwenye umri mdogo Mbwana Samata, ambaye huichezea TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na ambaye alikuwa ametupwa nje na
kocha wa awali Jan Poulsen. Wachezaji wengine walioalikwa kujiunga na timu
ya taifa kwa mara ya kwanza miongoni mwa vijana waliopo katika timu ya
chini ya umri wa miaka 20 ni pamoja na Ramadhani Singano, Edward
Christopher na Frank Domayo. "Kuna matumaini siku zijazo kupitia timu hii, na ninaamini mchezo wao utastawi na kustawi", alielezea Poulsen. Kikosi kitaanza mazoezi yake kikiwa kambini
kuanzia Jumatano, kwa nia ya kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya
Malawi, tarehe 26 mwezi huu wa Mei.
Kikosi cha Tanzania kina wachezaji;
Kipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam), Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar)
Walinzi: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey
Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani
(Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso
(Simba)
Kiungo cha Kati: Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum
'Sure Boy' Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba),
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba), Mrisho Ngasa
(Azam) Frank Domayo (JKT Ruvu)
Washambulizi: Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu
(TP Mazembe, DR Congo), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Moro
United), Haruna Moshi (Simba), John Bocco (Azam)
0 comments:
Post a Comment