Rais
Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa
muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao
wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja .Rais Obama
ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na idhaa ya kiingereza ya BBC.Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani
wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha
Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema
wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni
yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za
jinsia moja.
Kauli
ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina
kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni
muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.
0 comments:
Post a Comment