Rais Mstaafu Tanzania Benjamin William Mkapa amefika
mbele ya mahakama akiwa ni shahidi wa kwanza upande wa utetezi katika
mashataka yanayomkabili aliyewahi kuwa balozi waTanzania nchini Italia
Profesa Costa Mahalu.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi aliyewahi
kushika madaraka makubwa nchiniTanzaniakufika mbele ya mahakama
akitakiwa kutoa ushahidi upande wa utetezi dhidi ya ya tuhuma
zinamzomkabili mmoja wa watumishi katika kipindi cha utawala wake. Katika Mahakama ya hakimu mkazi ya
kisutu iliyojaa watu wengi Rais huyo mstaafu mara baada ya kuapa
ameieleza mahakama kuwa serikali yake ilifahamu na kisha kuridhia
ununuzi wa nyumba au jengo la ubalozi waTanzania nchini Italia baada ya
kushauriana na Balozi waTanzanianchini Italia wakati huo Profesa Costa
Mahalu. Hatua hiyo ilifuatia kuthaminiwa kwa jengo
lenyewe kulikofanywa na Mamlaka husika kutoka serikali yaTanzania.
Baadaye jengohilolilinunuliwa na Bw Mkapa kulizidnua rasmi alipokuwa
ziarani kikazi nchini Italia Mwezi February mwaka 2003. Akijibu swali la wakili upande wa mashtaka ni
kwa nini malipo ya shilingi Bilioni mbili na milioni 900 yakafanyika kwa
kupitia akaunti mbili tofauti,Bwana Mkapa ameiambia mahakama hiyo kuwa
alijulishwa kuwa hilo lilikuwa sharti na muuzaji nyumba na hivyo kwa
upande wa serikali hakuona kama kuna tatizo akizingatia kuwa thamani ya
jengo iliishafanywa na kuwaridhisha wao kama serikali huku kukiwa na
mahitaji makubwa ya Serikali ya Tanzania kuwa na majengo ya kudumu
ambayo yangemilikiwa na serikal.
Mmoja wa mawakili ambaye alimuongoza Bwana
Makapa kutoa ushahidi wake Wakili Alex Mgongolwa alimweleza mwandishi wa
BBC Eric Nampesya mjini Dar es salaam kuwa amefurahia kumuongoza Bwana
Mkama kutoa ushahidi wake mahakamani. Alisema ‘kitendo cha Rais mstaafu
kufika mahakamani kama shahidi kwa upande mwingine kimeonyesha ni jinsi
gani misingi ya sheria inaheshimiwa wakiwemo kiongozi wastaafukamaBwana
Benjamin Mkapa. Bw Mkapa akiwa na viongozi wengine wa Afrika. Kiongozi huyo anakuwa wa kwanza katika historia
yaTanzaniakwa miaka zaidi ya hamsini kwa kiongozi aliyewahi kuwa Rasi
kufika mbele ya mahakama na kutoa ushahidi. Katika kesi hiyo Balozi huyo wa zamani wa
Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu anashtakiwa kwa kuhujumu
uchumi ambapo inadakiwa kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu bei halisi
ya jengo la ubalozi lililonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa kutaja
bei ya juu, ikiwa ni tofauti na bei yake halisi. Prof Costa Mahalu anadaiwa kuisababishia
serikali ya Tanzania hasara ya $ 3.098 milioni (shilingi bilioni 2 na
milioni 900 za Tanzania).
0 comments:
Post a Comment