Pages

Pages

Tuesday, May 8, 2012

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa atoa Ushshidi mahakamani...

Rais Mstaafu Tanzania Benjamin William Mkapa amefika mbele ya mahakama akiwa ni shahidi wa kwanza upande wa utetezi katika mashataka yanayomkabili aliyewahi kuwa balozi waTanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi aliyewahi kushika madaraka makubwa nchiniTanzaniakufika mbele ya mahakama akitakiwa kutoa ushahidi upande wa utetezi dhidi ya ya tuhuma zinamzomkabili mmoja wa watumishi katika kipindi cha utawala wake. Katika Mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu iliyojaa watu wengi Rais huyo mstaafu mara baada ya kuapa ameieleza mahakama kuwa serikali yake ilifahamu na kisha kuridhia ununuzi wa nyumba au jengo la ubalozi waTanzania nchini Italia baada ya kushauriana na Balozi waTanzanianchini Italia wakati huo Profesa Costa Mahalu. Hatua hiyo ilifuatia kuthaminiwa kwa jengo lenyewe kulikofanywa na Mamlaka husika kutoka serikali yaTanzania. Baadaye jengohilolilinunuliwa na Bw Mkapa kulizidnua rasmi alipokuwa ziarani kikazi nchini Italia Mwezi February mwaka 2003. Akijibu swali la wakili upande wa mashtaka ni kwa nini malipo ya shilingi Bilioni mbili na milioni 900 yakafanyika kwa kupitia akaunti mbili tofauti,Bwana Mkapa ameiambia mahakama hiyo kuwa alijulishwa kuwa hilo lilikuwa sharti na muuzaji nyumba na hivyo kwa upande wa serikali hakuona kama kuna tatizo akizingatia kuwa thamani ya jengo iliishafanywa na kuwaridhisha wao kama serikali huku kukiwa na mahitaji makubwa ya Serikali ya Tanzania kuwa na majengo ya kudumu ambayo yangemilikiwa na serikal.
Mmoja wa mawakili ambaye alimuongoza Bwana Makapa kutoa ushahidi wake Wakili Alex Mgongolwa alimweleza mwandishi wa BBC Eric Nampesya mjini Dar es salaam kuwa amefurahia kumuongoza Bwana Mkama kutoa ushahidi wake mahakamani. Alisema ‘kitendo cha Rais mstaafu kufika mahakamani kama shahidi kwa upande mwingine kimeonyesha ni jinsi gani misingi ya sheria inaheshimiwa wakiwemo kiongozi wastaafukamaBwana Benjamin Mkapa. Bw Mkapa akiwa na viongozi wengine wa Afrika. Kiongozi huyo anakuwa wa kwanza katika historia yaTanzaniakwa miaka zaidi ya hamsini kwa kiongozi aliyewahi kuwa Rasi kufika mbele ya mahakama na kutoa ushahidi. Katika kesi hiyo Balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu anashtakiwa kwa kuhujumu uchumi ambapo inadakiwa kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu bei halisi ya jengo la ubalozi lililonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa kutaja bei ya juu, ikiwa ni tofauti na bei yake halisi. Prof Costa Mahalu anadaiwa kuisababishia serikali ya Tanzania hasara ya $ 3.098 milioni (shilingi bilioni 2 na milioni 900 za Tanzania).

No comments:

Post a Comment