Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel ‘AIRTEL SUPA 5’ itakayotoa ofa
tano kuwafaidisha wateja kuongea kwa NUSU Shilingi kwa sekunde siku
nzima kwa marafiki Airtel-Airtel, pia wateja wote wataongea kwa ROBO
Shilingi kwa sekunde usiku kucha Airtel-Airtel, kujipatia SMS 200 Bure
Siku Nzima endapo mteja atatuma SMS10 tu kwa 30Tshs, facebook burepamoja na kuburudika intaneti ya bure usiku mzima kwa wateja wote.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Rahma
Mwapachu akifafanua jambo jinsi ya kupata facebook bure kupitia ofa za
AIRTEl SUPA 5 mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani). Hafla hiyo ya uzinduzi huo umefanyika leo
katika ofisi za Airtel Makao makuu, Ili
mteja uweze kuingia na kutumia huduma hii unatakiwa kujiunga kwa kupiga
*149*99#. Kisha utapata ujumbe utakaokuhitaji kuchagua muda maalum wa
kutumia OFA hii yaani WIKI MOJA au SIKU MOJA, alafu utaweza kujaza namba
zako maalum 3 za ndugu, jamaa, au rafiki utakazotaka kuwa unazipigia
simu kwa NUSU shilingi siku nzima ndani ya muda wako wa ofa, Mbali
na hilo huduma hii ya SUPA 5 inatoa nafasi kwa mteja yeyote wa malipo
ya kabla wa Airtel ambaye amejiunga lakini pia muda wake ukiisha anaweza
kujiunga tena kwa mara nyingine, lengo ni kumpa mteja wa Airtel nafasi
ya kujiachia kwa unafuu na uhakika zaidi muda wowote na sehemu yoyote
nchini Tanzania. Huduma
ya Airtel SUPA 5 ni ya kudumu, lengo lake ni kutimiza mahitaji ya
wateja wetu nchini bila kujali aina ya simu anayotumia huku tukitoa
mawasiliano bora kupitia mtandao wetu ulionea kila mahali nchini
Tanzania.
Jiunge na OFA hii ya Airtel SUPA 5 kwa kupiga *149*99#.
No comments:
Post a Comment