Wahandisi wanasema mkongo huo uliharibiwa na meli ilioshusha nanga yake katika eneo ambalo hairuhusiwi, Kutokana na kisa hicho kampuni za kutoa huduma
za mawasiliano ya internet zimekuwa zikitoa huduma hiyo kwa viwango vya
kasi ndogo kuliko inavyohitajika. Joel Tanui, msemaji wa kampuni ya The East
African Marine Systems (Teams), amesma majaribio yao yanaonyesha kuwa
mkongo huo unaounganisha ukanda huu na dunia nzima umekatika kabisa. Bw Tanui ameelezea kuwa kutokana na hilo huduma
za mawasiliano kutumia internet zimeathirika nchini Kenya, Uganda,
Tanzania, rwanda, Burundi, ethiopia and Sudan kusini. Huduma hizo ingawa
zinapatikana kwa sasa sio kwa kasi inayohitajika.
Mkongo mwengine wa mawasiliano unaomilikiwa na
kampuni ya East African Submarine cable systems (EASSy) ambao
unaunganisha nchi zilizoko kusini na kaskazini mwa Afrika na dunia nzima
pia nao ulikatwa na meli hiyo.
Uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo ambapo meli iliruhusiwa kushusha nanga yake katika eneo ambalo hairuhusiwi.
Kazi ya kurekebisha mkongo huo itachukua muda wa wiki mbili, kulingana na msemaji wa Kampuni ya TEAMS.
Kisa hicho kimeathiri sana shughuli na biashara
zinazotegemea sana huduma ya mtandao wa internet kote mjini Nairobi.
Hasaa Kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi ambazo zimekuwa
zikichuma kupitia huduma ya internet tangu mkongo huo wa mawasiliano
uzinduliwe.
Mkongo huo wa mawasiliano ulizinduliwa mwaka wa
2009 ukiwa ni ubia kati ya serikali ya Kenya na idara ya mawasiliano za
miliki za Emirati.
Huduma hiyo ilipunguza gharama za internet
maradufu kwani kabla ya hapo kampuni nyingi zilitegemea satelite kutoa
huduma hiyo, njia ambayo ni ghali mno.
No comments:
Post a Comment