Timu ya Taifa 'Taifa Stars' leo imeshindwa kutamba mbele ya Malawi
katika mchezo wa kujipima nguvu kabla ya michezo ya kusaka tiketi ya
kombe la dunia mwaka 2014 ambapo Taifa Stars itwakwaana na Ivory Coast
na Malawi kuwavaa Waganda. Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam na mchezo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana huku Taifa Stars
wakifanya makosa ambayo yange igharimu timu hiyo hii leo kama Malawi
wangekuwa Makini. Taifa Stars walicheza kiuwelewano katika kipindi cha kwanza na huku
wakitengeneza nafasi chache za kujipatia magoli wakati wa Malawi
walionekana kuwa hatari kwa mipira mirefu. Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa stars ambapo kuungo chake kilipotea
na kadri ya dakika zilivyosogea wachezaji walionekana kuchoka. Nafasi pekee ambayo Stars wameijutia kuipoteza ilikuwa katika dakika ya
58 ambapo Shomari Kapombe na Mbwana Samata waligusiana vyema na mpira wa
mwisho kumkuta Samata ambaye aliingia na mpira kwenye eneo la hatari
akitokea upande wa kulia na alipo piga pasi ya chini chini kuelekea kwa
Haruna Moshi 'BOBAN' ambapo beki wa Malawi ulimgonga na kwenda kugonga
mwamba wa pembe ya pili na mpira kuamba katikati ya Boban na Ngassa
kabla ya beki wa Malawi kuutoa nnje na kuwa kona. Na nafasi pekee ambayo wa Malawi wanaweza jutia ni ile ya kipindi cha
kwanza ambapo Juma Kaseja alielekea upande sio baada ya Yondan kuhamisha
muelekeo mpira katika purupushani ya kuokoa na mpira kumkuta
mshambuliaji wa Malawi aliyepiga kichwa na mpira wake kuokolewa na
Aggrey Morise.
No comments:
Post a Comment