Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa shule za sekondari 24, Kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya vijana chini ya miaka 17 maarufu kama ''Airtel Rising Star''. Inayotarajiwa kuanza Mei 30, Lengo kubwa ni kuinua vipaji kwa vijana wenye chini ya miaka 17. Akikabidhi vifaa hivyo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) Sanifu Kondo, Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde,
alisema jumla ya timu 24 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo. Alisema vifaa vilivyotolewa ni jezi na mipira na kila timu itapatiwa jezi mbili.
"Mwaka
huu tumeboresha zaidi michuano hii ikiwa ni pamoja na kushirikisha
timu za wasichana tofauti na hapo awali, ambapo kila mkoa utatoa timu ya
wanawake ambayo itakuwa kombaini.
"Mwaka huu mashindano
yatashirikisha mikoa sita kwa kuanzia ngazi ya mikoa kabla ya ile ya
taifa itakayoanza Juni na timu bingwa itashiriki mashindano ya siku nne
nchini Kenya yajulikanayo kama Inter Continental Tourmament
yatakayoshirikisha mataifa zaidi ya 16," alisema Jane. Alisema
mbali na timu hiyo pia watateua wachezaji sita bora ambao watashiriki
kliniki ya soka maarufu kama Coaching Stars itakayofanyika nchini Kenya
chini ya jopo la makocha kutoka Academy ya soka ya Manchester United ya
Uingereza.
No comments:
Post a Comment