Pages

Pages

Saturday, April 28, 2012

Rais wa Malawi amfuta kazi hasimu wake

Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika, kakake Marehemu Rais Bingu Wa Mutharika aliyefariki dunia mwezi huu.
Mutharika alitarajiwa kurithi Marehemu Kakake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 ambapo Bingu Wa Mutharika alitarajiwa kustaafu.
Mabadiliko ya baraza la mawaziri yametokea siku chache baada ya maziko ya Rais huyo mapema wiki hii. Bi. Banda amekuwa Makamu wa Rais tangu mwaka 2009 lakini akatofautiana na Wa Mutharika na kuwa mkosoaji wake mkubwa.
Kufuatia kifo cha Rais huyo kulizuka wasi wasi kwamba wandani wake wangejaribu kuzuia ukabidhi wa madaraka kwa Bi. Banda ambaye alikuwa na chama chake cha kisiasa.
Miongoni mwa Mawaziri wapya ni Austin Atupele Muluzi, mwanawe Rais wa zamani Bakili Muluzi aliyeteuliwa Waziri wa mipango na ustawi.Wengi waliotimuliwa na waliokuwa wandani wa Bingu Wa Mutharika.

No comments:

Post a Comment