Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa,
akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na
wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa
wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati
wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye
thamani ya milioni 25/- TZS toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel
kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Chuo
kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi mwaka
2007 huku kikiwa na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library) kuliko
chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo hicho
kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku matarajio ni
kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa siku zijazo.
No comments:
Post a Comment