Bw Taylor ndiye kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukabiliwa na hukumu
mbele ya Mahakama ya Kimataifa tangu kesi maarufu za Nuremburg baada ya
vita vikuu vya pili vya Dunia. Atahukumiwa mwezi ujao.
Charles Taylor alikua Rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi
alipojiuzulu mnamo mwaka 2003 kufuatia shinikizo kali za kimataifa.
Alianza shughuli za siasa wakati wa ziara yake nchini Liberia kama
kiongozi wa msafara wa mashirika ya Waliberia yaliyo barani Amerika
mapema katika muongo wa 1980, mapinduzi ya kijeshi yalipofanyika naye
kupewa kazi katika serikali ya Samuel Doe.
Baada ya kuteuliwa kama Naibu waziri katika
Wizara ya biashara ya serikali ya Rais Doe, Taylor aliikimbilia Marekani
kufuatia madai kwamba amepoteza takriban dola za kimarekani milioni
moja.
Alifungwa huko Marekani lakini akatoroka jela
katika mazingira ambayo hadi leo bado ni ya kutatanisha. Hatimaye
aliunda kundi lake la waasi, lililojulikana kama National Patriotic
Front of Liberia, ambalo liliiondoa serikali ya Samuel Doe madarakani.
Taylor ana kipaji cha kua mtu mchangamfu ambaye aliweza kumbadili
adui na kumpenda kiasi cha kumfanya kua mfuasi sugu. Kwa mfano
alipoingia mji wa Monrovia mnamo mwaka 1995 makumi kwa mamia ya watu
waliompinga walijitokeza kumpokea na kumuimbia nyimbo za kumsifu kama
shujaa.
Licha ya kuwateua watu wengi kama washauri wake
lakini hiyo ilikua danganya toto'' kwa sababu hakufuata ushauri wao hata
siku moja. Mmoja wa washauri wake wa karibu aliwahi kuniambia kua
yaliyomfika Taylor yangeweza kuepukika kama angewasikiliza washauri hao.
Taylor alipenda sana kujifananisha na watawala
wa enzi ya karne ya kumi na tisa kwa jinsi alivyowazawadia fukara
akifahamu kua fadhila zake zitamjengea sifa na kumfaa siku moja.
Akiwa mpenda madaha alifahami vyema nguvu ya
vyombo vya habari na jinsi ya kuvitumilia. Kupitia miaka ya 1990
alishiriki mahijiano mengi ya kipindi cha BBC cha Focus on Africa.
Katika kipindi cha kwanza, akiwa ni kiongozi wa kundi la waasi asiyefahamika, alitangaza mpango wake wa kuivamia Liberia.
Miaka michache baadaye, alipodokezewa na
mtangazaji kwamba watu wengi wanamuonelea kua muuwaji, alilipuka na
kusema ''Hata Yesu Kristu alituhumiwa kua ni muuwaji enzi zake.
Katika mahojiano mengi aliyofanya daima
alijitahidi kudhibiti mahojiano ili kutoa sura inayompendeza yeye. Mfano
uilipomrushia suali lililomchukiza alijitahidi kulibadili liweze
kusikika kwa manufaa yake.
Kama mpiganaji mahiri alijivunia uwezo wake wa
kiume na uwezo wa kuzaa watoto wengi. Hakuficha siri yake ya kupenda
wanawake, akidokeza wakati mmoja kua kama kiongozi wa Kiafrika ana haki
ya hadi wake wanne.
Mwanamitindo Naomi Campbell alihusishwa katika kesi ya Taylor
Wakosoaji wake walipokashifu tabia yake ya
uzinzi, alijibu kwa kuwakemea wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja
na kujibu ''Bora mimi nawapenda wanawake.''
Mnamo mwaka 1996 alidokezea kua angetaka
kujaliwa na watoto wengine watano na wote watakua wanaume. Hata hivyo
hakujaliwa na ndoto yake hio watoto wake wawili waliofuata walikua wa
kike.
Labda kama ishara ya kujiliwaza majaliwa hayo,
aliwahi kusema kua kama mzazi anayewapenda wanawe, mume yeyote
atakayewaoa wanangu, itabidi akubali watoto wake warithi jina la Taylor
liendelee kudumu katika familia
No comments:
Post a Comment