Zitto Kabwe-Bunge halina mguso na wananchi 'out of touch'
Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala
mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta
Afya. Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali
kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika
akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa.
Bunge lika...ahirishwa
siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya
Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja
kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.
Leo wabunge kwa mara
nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge
akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge
hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la
Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.
Hii inadhihirisha
kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi
ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch). Hali hii ni
hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi
kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo
kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge liache shughuli nyingine zote na
kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari,
kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.
No comments:
Post a Comment